Kuwasaidia waathiriwa wa tetemeko la ardhi
Zaidi ya watu 4,800 kutoka Uturuki na Syria walipokea makazi ya muda bila malipo.
Dhamira ya Airbnb.org ni kufungua uwezo wa kushiriki sehemu, nyenzo na usaidizi wakati wa uhitaji.
Kutana na jumuiya yetu
Kupitia jumuiya yetu ya kimataifa ya Wenyeji, wafadhili na mashirika washirika, Airbnb.org iliweza kuwapa watu zaidi ya 140,000 makazi ya muda.
Jinsi Carmen na jumuiya yake walivyoungana baada ya Kimbunga Maria.
Tunazipa jumuiya njia ya kuja pamoja majanga yanapotokea. Kupitia mipango ya Airbnb.org, watu wanaweza kutoa nyumba zao bila malipo kwa majirani ambao wanahitaji kuhamishwa.
Airbnb.org imewasaidia zaidi ya watu 135,000 wanaokimbia vita kupata sehemu za kukaa.
Inaweza kuchukua miaka kwa jumuiya kupona kabisa kutokana na janga kubwa. Airbnb.org husaidia kufadhili sehemu za kukaa kwa wafanyakazi wa misaada ambao wanafanya kazi muhimu ya kujenga upya jumuiya.
Kuunda ulimwengu uliojikita katika kujisikia nyumbani
Airbnb.org inatazamia ulimwengu ambao mtu yeyote anaweza kupata sehemu ya kukaa inayomfanya ahisi amekaribishwa wakati wa mgogoro. Ili kufanikisha maono haya kwa kila mtu, Airbnb.org iliunda ahadi kadhaa kuhusu uanuwai, usawa, ujumuishaji na ufikiaji.