Els ni Mwenyeji huko Rome ambaye alikaribisha mkimbizi kupitia Airbnb.org.

Saidia kuwapa makazi wakimbizi 100,000 wanaokimbia kutoka nchini Ukrainia

Toa sehemu za kukaa bila malipo au kwa punguzo kupitia Airbnb.org au uchangie ili kusaidia fedha zetu zitimize mengi zaidi.

Usaidizi wako huleta tofauti

Airbnb.org inafadhili makazi ya muda mfupi kwa hadi watu 100,000 wanaokimbia Ukrainia. Tunawasaidia wageni wetu wakimbizi bila kujali utaifa, mbari, kabila au jinsi wanavyojitambulisha.

Unaweza kutoa msaada kwa kutoa sehemu za kukaa za muda bila malipo au kwa punguzo kupitia Airbnb.org au kutoa mchango ili kufadhili sehemu za kukaa.

Linda, Mwenyeji huko Dallas, amewakaribisha wakimbizi kupitia Airbnb.org.

Toa sehemu ya kukaa

Anza kukaribisha wageni bila malipo au kwa punguzo.

Namna kukaribisha wageni kunavyofanya kazi

  • Utatoa kitanda cha starehe na vistawishi vya msingi kwa ajili ya mahali popote kuanzia siku kadhaa hadi wiki kadhaa. Pata maelezo zaidi kuhusu kukaribisha wageni wakimbizi
  • Airbnb.org inashirikiana na mashirika yasiyotengeneza faida ambayo huwakagua wageni wakimbizi ili kuona kama wanastahiki na kuwasaidia kabla ya ukaaji wao, wakati wa ukaaji wao na baada ya hapo.
  • Airbnb inawapa Wenyeji AirCover: bima ya dhima ya USD milioni 1, ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3 na kadhalika, bila gharama kwa Wenyeji. Vikomo na vighairi fulani hutumika.
Fode ni mgeni mkimbizi ambaye alikaa na Mwenyeji nchini Italia kupitia Airbnb.org.

Kila mchango husaidia kutimiza uhitaji muhimu wa sehemu za kukaa za dharura kwa wale wanaokimbia nchi ya Ukrainia na wengine walio katika shida.

Jinsi kutoa mchango kunavyofanya kazi

  • Asilimia 100 ya mchango wako utatumiwa kuwawezesha watu kupata makazi ya muda mfupi.
  • Sehemu za kukaa hazina malipo kabisa kwa wageni walio kwenye mpango wetu.
  • Michango inatozwa kodi kwa kiwango kinachoruhusiwa chini ya sheria za kodi za eneo lako.
Josue hukaribisha wageni kupitia Airbnb.org ili kuwakaribisha watu wanaokimbia majanga ya aina nyingi.

Je, unahitaji usaidizi?

Hatutoi makazi moja kwa moja kwa watu binafsi kwa wakati huu. Airbnb.org hushirikiana na washirika wengine wasiotengeneza faidia ambao huweka nafasi na kuratibu sehemu za kukaa kwa ajili ya wageni wakimbizi.

Kile ambacho washirika wetu wasiotengeneza faida hufanya

Washirika wetu ni mashirika yasiyotengeneza faida ambayo husaidia kuwakaribisha wakimbizi. Mashirika haya yanasaidia wateja wao kupata makazi na kadhalika. Mapendekezo kutoka kwa mashirika yasiyotengeneza faida yanakubaliwa kwa mwaliko tu.

Kile ambacho Airbnb.org inafanya

Airbnb.org hutoa ruzuku na teknolojia kwa washirika wetu wasiotengeneza faida, ambao huratibu makazi ya muda kwa ajili ya wateja wao.

Washirika wetu

  • HIAS
  • Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)

Jinsi Airbnb inavyotoa michango

Kuwasaidia Wenyeji

Airbnb inawapa Wenyeji AirCover: bima ya dhima ya USD milioni 1, ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3 na kadhalika, bila gharama kwa Wenyeji. Vikomo na vighairi fulani hutumika.

Kufadhili sehemu za kukaa

Airbnb na wafadhili wanachangia fedha kwa ajili ya sehemu za kukaa za muda kwa hadi wakimbizi 100,000 wanaokimbia Ukrainia.

Kusamehe ada

Airbnb inasamehe ada za Wenyeji na wageni kwenye sehemu zote za kukaa za Airbnb.org kwa ajili ya wakimbizi.