Kutoa msaada wakati wa shida
  • Kuwasaidia waathiriwa wa tetemeko la ardhi

    Zaidi ya watu 4,800 kutoka Uturuki na Syria walipokea makazi ya muda bila malipo.

Dhamira ya Airbnb.org ni kufungua uwezo wa kushiriki sehemu, nyenzo na usaidizi wakati wa uhitaji.

Tumetoa zaidi ya usiku milioni 1.4 katika sehemu za kukaa za dharura bila malipo kwa zaidi ya watu 220,000 tangu kuanzishwa kwetu mwaka 2020.

Kutana na jumuiya yetu

Wenyeji na wageni wa Airbnb.org ndio kiini cha dhamira yetu.

Kupitia jumuiya yetu ya kimataifa ya Wenyeji, wafadhili na mashirika washirika, Airbnb.org iliweza kuwapa watu zaidi ya 140,000 makazi ya muda.

Jinsi Carmen na jumuiya yake walivyoungana baada ya Kimbunga Maria.

Tunazipa jumuiya njia ya kuja pamoja majanga yanapotokea. Kupitia mipango ya Airbnb.org, watu wanaweza kutoa nyumba zao bila malipo kwa majirani ambao wanahitaji kuhamishwa.

Airbnb.org imewasaidia zaidi ya watu 135,000 wanaokimbia vita kupata sehemu za kukaa.

Inaweza kuchukua miaka kwa jumuiya kupona kabisa kutokana na janga kubwa. Airbnb.org husaidia kufadhili sehemu za kukaa kwa wafanyakazi wa misaada ambao wanafanya kazi muhimu ya kujenga upya jumuiya.

Kuunda ulimwengu uliojikita katika kujisikia nyumbani

Airbnb.org inatazamia ulimwengu ambao mtu yeyote anaweza kupata sehemu ya kukaa inayomfanya ahisi amekaribishwa wakati wa mgogoro. Ili kufanikisha maono haya kwa kila mtu, Airbnb.org iliunda ahadi kadhaa kuhusu uanuwai, usawa, ujumuishaji na ufikiaji.

Tunasaidia mashirika mengine yasiyotengeneza faida kuleta matokeo ya kudumu.

Kutana na washirika wachache waliosaidia kuunda Airbnb.org.
IRC hukabiliana na majanga mabaya zaidi ya kibinadamu ulimwenguni na huwasaidia watu ambao maisha na riziki yao imeharibiwa na mizozo na maafa ili waweze kuishi, kurudia hali yao ya kawaida na kupata udhibiti wa maisha yao ya baadaye.
Build Change ni shirika la kuzuia na kukabiliana na majanga linalounda suluhisho za makazi bora pamoja na jumuiya za eneo husika.
HIAS ni shirika lisilotengeneza faida la Kiyahudi ulimwenguni ambalo hutoa ulinzi na msaada kwa wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na watu wengine waliohamishwa kwa nguvu ulimwenguni kote.
Community Sponsorship Hub inajenga fursa kwa jumuiya mbalimbali kote nchini Marekani kuwakaribisha wakimbizi na watu wengine waliofukuzwa kutoka makazi yao.